š‘±š‘°š‘µš‘ŗš‘° š’€š‘Ø š‘²š‘¼š‘±š‘Ø š‘µš‘Ø š‘¾š‘Øš’š‘¶ š’š‘¼š‘¹š‘° š‘³š‘Ø š‘©š‘°š‘Øš‘ŗš‘Æš‘Øš‘¹š‘Ø.



Ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kuwa na wazo zuri la biashara. Je unajua jinsi ya kupata wazo hilo zuri la biashara? 

Watu wengi wamekuwa wakiniomba ushauri ni wazo gani zuri la biashara ambalo linaweza kuwapatia faida na mafanikio. Ukweli ni kwamba wazo ambalo ni bora kwa mtu fulani linaweza lisiwe bora kwako.

Moja ya sababu zinazofanya biashara nyingi kufa au kutokuendelea ni kuiga, yaani mtu akianza biashara leo baada ya muda unakuta watu wengine wameiga biashara ile ile, wanaifanya eneo lile lile na kwa mbinu zile zile. Hii ni njia rahisi sana ya kushindwa kwenye biashara.

Kuja na wazo la biashara kuna mambo mengi sana ya kuzingatia, hii ni pamoja na upo eneo gani, mkoa gani, elimu yako, watu waliokuzunguka, ujuzi, umri wako, muda, mtaji, resources, njaa yako, kiu ya kufanikiwa, connection, etc

Hivyo hakuna formula moja ambayo utatumia. Hapa chini nimejaribu tu kukupa njia mbali mbali kama muongozo. Unaweza chagua njia yoyote na kuanza nayo. Pia bilakusahau unaweza pitia uzi huu ukakuongezea madini

TUMIA UJUZI ULIO NAO

Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiriwa na ni fundi seremala, kwa nini usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo?

BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA

Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu hupata mafanikio, kama wewe hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usifundishe watu kuogelea?

Kuna njia mbali mbali unaweza tumia kuanzisha biashara kutokana na hobby yako pitia uzi huu

NUNUA BIASHARA AMBAYO TAYARI IPO

Ukishindwa kabisa kupata wazo zuri unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizi kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua na kuendelea nayo. Kuna vigezo vya kuangalia kabla ya kununua.

NINI KINAKOSEKANA MTAANI?

Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani, geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenu au maeneo unayo kwenda kustarehe.

-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?

Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?

Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?

Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirani huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

Ni tatizo gani sugu ambalo wewe mwenyewe hua linakusumbua na hujapata solution?


Ni kitu gani umeona inaweza kua tatizo mbeleni? Mfano kwa sasa watu wanakula junk food bila kuangalia afya zao hili ni tatizo unaweza kuja na solution yake

Huduma au bidhaa gani inaweza kuokoa pesa/muda wa mteja wako mtarajiwa?

Huduma gani inaweza rahisisha maisha ya mtu?

ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA WANAHITAJI NINI?

Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji.

UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE

Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza. Fanya utafiti kabla ya kuanza kuuza bidhaa hizi. Mfano miezi miwili mitatu nyuma kuna mafuta ya wanawake yanaitwa Snail yameuzwa sana. Hii ilikua bidhaa nzuri

ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI

Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, kitaifa na kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango wakutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO

Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika

TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA

- Maonyesho ya biashara

- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara

- Kwa marafiki.

MITANDAO YA KIJAMII

Watu kwenye mitandao ya kijamii ni rahisi sana kupost kuhusu matatizo na kero zao kuhusu huduma au bidhaa flani. Wachache hua wanafuatilia na kutatua matatizo hayo. Matatizo hayo yanaweza kua chanzo cha wazo bora la biashara.

WEBSITE ZA BIASHARA

Kuna kurasa za Instagram ambazo hua wanauza vitu mbali mbali au mitandao kama ebay, AliExpress, AliBaba, Kikuu, Inalipa, etc pendelea kuitembelea na kuangalia bidhaa zinazouzwa humo ni chanzo kizuri cha mawazo ya biashara

TEMBELEA MASOKO MAKUBWA

Kwa kutembelea masoko makubwa kama Kariakoo na mengine kama hayo. Yanaweza kukufungua akili kufahamu biashara gani ya kufanya. Kwa kuangalia bidhaa aina gani zinatoka au wateja wanazikimbilia.

UNAWEZA GUNDUA KITU?

Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama kuna jamaa nilimuona TBC katengeneza mashine zake za kukunia nazi kwa umeme. Jamaa anauza mashine 300,000 mashine hizo nikakuta kariakoo vijana wanatumia kukunia nazi moja 200. Kwa siku jamaa wanakuna nazi hadi 500

Kama tulivyoona hapo juu hizo ni baadhi tu ya njia unazoweza kuzifanya ukiwa unatafuta wazo la biashra. Kama kunayoyote nimeisahau unawea kuiongezea hapa chini. Vitu 20 vya kuzingatia wakati unatafuta wazo la biashara.


š‘°š‘³š‘° š‘¾š‘Øš’š‘¶ š‘³š‘Øš‘²š‘¶ š‘³š‘Ø š‘©š‘°š‘Øš‘ŗš‘Æš‘Øš‘¹š‘Ø š‘³š‘°š‘­š‘Øš‘µš‘°š‘²š‘°š‘¾š‘¬ š‘½š‘°š‘»š‘¼ š‘½š’€š‘Ø š‘²š‘¼š’š‘°š‘µš‘®š‘Øš‘»š‘°š‘Ø:

Vitu vingine vya kuzingatia wakati unakuja na wazo lako la biashara.

Yes unaweza fungua biashara kutokana na kitu unachokijua mfano Kinyozi ukafungua saluni yako au mpishi ukafungua restaurant yako. Kumbuka kwakua wewe ni mpishi mzuri sio kwamba utafahamu jinisi ya kuendesha restaurant yako vizuri. Kuna mambo mengi ya kuzingatia

Kama unataka biashara endelevu make sure huduma au bidhaa unayouza wateja wako watarudi kwako tena. Inabidi uwe na bidhaa au huduma ambayo wateja wataendelea kununua kwa muda mrefu. Mfano ni bora uwe na kampuni ya kusafisha swimming pool kuliko kua na kampuni ya ujenzi wa pool.

“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.” Nafikiri ushawahi kusikia huu msemo. Mimi nitaweka msistizo tu sio kila unachokipenda kinaweza kua biashara yenye faida. Yes fanya unachokipenda but angalia kama kinaweza kua biashara yenye faida.

Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.

Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu

Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.

Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.

Wataalamu wa biashara wanashauri ili uanze biashara inabidi uwe na Unique Selling Proposition (Utafauti katika soko) Bidhaa zako au huduma ziwe tofauti na washindani wako. Hii ni changamoto na inaweza kukwamisha, sio lazima bidhaa yako au huduma iwe tofauti.

Kuna baadhi ya bidhaa hazina USP, Badala ya kutafuta USP ya huduma au bidhaa yako tafuta jinsi gani utaiuza kiutofauti

Je una ujuzi au resources ambazo zinaweza kukusaidia kufanya wazo lako la biashara kua na faida? Kama hauna jifunze mpaka uwe na ujuzi au uwezo wa kufanya. Mfano nimeona kuna fursa nyingi kwenye graphics design na sina ujuzi huo, jifunze.

Zingatia swala la fedha

Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.

Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.

Angalia uhitaji wa soko

Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.

Tatua tatizo au changamoto ambayo mteja wako mlengwa anayo. Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.

Ushindani

Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.

Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza..

Wazo lako la biashara kabla ya kurukia na kuanza kufanya hakikisha umefanya utafiti wa kutosha na kikubwa umefanya majaribio kadhaa, Kuna njia za kufanya majaribio ya wazo lako la biashara, baadhi nimeelezea hapa

Kama nilivyoeleza hapo awali, uchaguzi wa wazo la biashara unahitaji utulivu na umakini mkubwa.

Usichague wazo kwa kuwa wengine wamelichagua au wengine linawapa faida; bali chagua lile linalokufaa wewe na mazingira yako.

@PingThread unroll

Post a Comment

0 Comments