Dondoo za Soka Afrika na Tetesi Za Usajili.

 


Mwandishi wa habari za michezo wa Ghana Nuhu Adams ameripoti kuwa Kiungo mshambuliaji wa Simba SC Luis Miquissone amekubali kujiunga na Al Ahly ya Misri baada ya kukataa ofa ya kujiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Klabu ya Medeama SC ya Ghana imeachana na Beki Zana Coulibaly raia wa Ivory Coast kwa makubaliano ya pande mbili. Zana mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na klabu hiyo February 2021 kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya As Vita Club August 2020 ambayo alijiunga nayo July 2019 akitokea Simba SC. Akiwa Medeama Zana alicheza mechi mbili tu ikiwa dakika 90 dhidi ya Great Olympics na dakika 58 dhidi ya Ashati Gold FC.


 TP Mazembe wanainyemelea saini ya mshambuliaji Raia wa Mali 'Zoumana Simpara'. Simpara (23) huenda akapewa kandarasi ya miaka 5 kama dili hilo litakamilika.

Klabu ya Horoya AC ya Guinea imetangaza kukamilisha usajili wa beki Issaka Samake raia wa Mali kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka klabu ya Stade Malien ya kwao Mali.


Mshambuliaji wa klabu ya Raja Casablanca ya Morocco, Ben Malango Ngita raia wa DR Congo ameondoka nchini Morocco kwenda Falme za kiarabu kwenda kujiunga na klabu ya Al Sharjah Sports. Ngita alishakubaliana na Al Sharjah kusaini mkataba wa miaka mitatu kwa mkataba wenye thamani ya dola milioni 3.5 (Zaidi ya Bilioni 8.1 za Kitanzania).

Klabu ya KCCA FC imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Brian Majwega kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya URA. Majwega mwenye umri wa miaka 28 hii ni mara yake ya tatu kucheza KCCA kwani alishawahi kucheza katika klabu hiyo 2009-2013 na 2015-2017.





Post a Comment

0 Comments