Fainali ya Ligi ya Mabingwa Africa kupigwa leo



CAFCL FINAL: CHIEFS VS AL AHLY.


Kaiser Chiefs ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆVS Al Ahly SC ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ Leo Saa 4:00 Usiku (EAT) Kwenye uwanja wa Stade Mohamed V, Casablanca Morocco๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ


______

Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imefika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao na kupata nafasi dhidi ya bingwa mtetezi anayeshikilia rekodi kushinda taji mara tisa, Al Ahly ya Misri.

Chiefs wamekuwa timu ya tatu kutoka Afrika Kusini kutinga fainali ya CafCL baada ya Mamelodi Sundowns (2001 & 2016) na wapinzani wao wakubwa Orlando Pirates (1995 & 2013).

Ni mafanikio makubwa kwa Kaizer Chiefs ambayo msimu huu wa ligi kuu nyumbani haikufanya vizuri baada ya kumaliza nafasi ya nane katika ligi yenye timu 16 wakiwa na alama 31 nyuma ya mabingwa Sundowns.

Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane pia aliwahi kushinda kombe la ligi ya Mabingwa akiwa na Mamelodi Sundowns mnamo 2016, sasa anakutana dhidi ya Kaizer Chiefs kutoka nchini mwake.

Fainali ya mwaka huu itakuwa ya mchezo mmoja (One Leg) utakaochezwa leo Julai 17 Saa 4:00 Usiku (EAT) huko Stade Mohammed V huko Casablanca, Morocco.

Post a Comment

0 Comments