Huu hapa usajili wa Azam mpaka sasa

 


KLABU ya Azam inaendelea kuonyesha makucha yake katika dirisha la usajili wa wachezaji wapya ambapo leo wamemtangaza rasmi, Kenneth Muguna na kufanya idadi ya nyota wapya waliosajiliwa na klabu hiyo mpaka sasa kufikia wanne.

Huu hapa usajili wa Azam mpaka sasa;

  1. Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Charles Zulu, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Cape Town City ya Afrika Kusini.
  2. Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco ya huko.
  3. Beki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama, kwa usajili huru akitokea Ruvu Shooting.
  4. Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Kenneth Muguna, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya huko.
  5. Kiungo wa kimataifa wa Zambia Paul Katema (23) kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Red Arrows ya Zambia.

Post a Comment

0 Comments