Kagame Cup 2021 Kufanyika Agosti 1-15 jijini Dar, Tanzania.



 Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limethibitisha kuwa Kombe la CECAFA, Kagame Cup 2021 litafanyika Agosti 1-15 jijini Dar, Tanzania.


Auka Gecheo, Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA alisema droo ya mashindano hayo itafanyika mnamo Julai 27. Huku timu ya Big Bullets ya Malawi itakuwa timu mwalikwa

Huku Simba SC mabingwa wa ligi kuu Tanzania na timu ambao walifika hatua ya robo fainali ya CAF 2020/2021 Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champion League) watakosa mashindano hayo hajajulikana ni sababu ipi klabu hiyo kutoshiriki mashindano hayo

Timu 10 ambazo zilizothibitishwa kushiriki mashindano ya Kombe la Kagame 2021:

1-Young Africans SC (Tanzania)
2-Azam FC (Tanzania)
3-Altabara FC (Sudan Kusini),
4-Le Messager FC (Burundi)
5-APR (Rwanda)
6-Express FC (Uganda)
7-KCCA FC (Uganda)
8-Tusker FC (Kenya)
9-KMKM SC (Zanzibar)
10-Big Bullets FC (Malawi).

Post a Comment

0 Comments