Kisa Yacouba Shabiki Simba Afariki Dunia

 


Shabiki wa Simba, Kilosa Said mwenye umri zaidi ya miaka 50 mkazi wa Kijiji Cha Mwamgongo Mkoani, Kigoma amefariki Jana wakati akiangalia mechi ya Simba na yanga.

Rafiki wa Marehemu, Msafiri Shibu, amesema tukio hilo lilitokea walipokuwa wakiangalia mchezo huo wa watani kwa njia ya Runinga eneo la Mwamgongo.

“Tulikuwa tunaangalia mpira eneo la Mwamgongo, tulitandika turubai chini tukawa tunaangalia mpira kwenye runinga wakati Mchezaji wa Yanga, Yacouba Songné anafanya shambulizi kwenye lango la Simba presha ikapanda.

“Tukamchukua na kumpeleka hospitali, akawa ameshapoteza maisha, presha yake ilikuwa 250, Marehemu ameacha Mke na Watoto wawili,” – Msafiri Shibu.

Kilosa anatarajia kuzikwa leo Julai, 26 saa 10, jioni katika kijini cha mwamgongo, mkoani Kigoma.

Post a Comment

0 Comments