KWAHERI YA KUONANA (Timu Zilizoshuka Daraja)



Rasmi sasa JKT TANZANI, IHEFU na GWAMBINA wanaungana na MWADUI Kushuka Daraja Rasmi Baada ya Michezo ya Mwisho ya Ligi Kuu Bara.

.

-JKT walikuwa na Timu imara nzuri, Pia Mwalimu Wao Abdalah Mohamed Baresi Ni mzoefu Pia hawana Shida au matatizo ya Kiuchumi Ila Kilichowaponza ni Kuishi Kwa Mazoea na Kuamini Ligi iko vikevike miaka yote jambo ambalo sio Sawa.


- IHEFU Wao Sera Yao Walioanza nayo Wakati wakianza Ligi iliwaangusha kiasi kwani walikuja na Sera ya kutosajili Sana Wachezaji wazoefu zaidi walisisitiza kuwa watatumia Sana vijana na Wale kadhaa Ambao walipanda Nao kutoka Daraja la Kwanza 


Wakapoteza Sana Mechi Raundi ya kwanza na wakaja kushtuka Raundi ya Pili wakasajili majina makubwa na wazoefu Akina Rafael Daudi, Dida, Mwasapili, Juma Mahadhi na wengine kibao pamoja na Mwalimu mzoefu Zubery Katwila ila Haikutosha kuwaokoa Siku za Mwisho Japo wamejitahidi Sana kupambana na kuwa Bora mzunguko Wa pili Ila ikashindikana Na Walikumbuka Shuka kukiwa kumeshakucha


- GWAMBINA Story Yao kiasi inafanana na Ihefu mbali ya wote kumilikiwa Na watu Wenye Uwezo pamoja na Kuwa na Viwanja vyao Binafsi Ila Eneo la kutokuwa na Wachezaji wengi Wenye uzoefu mwanzo Wa Ligi iliwaangusha Japo sio lazima uwe na wazoefu ili ufanye vizuri Ila tunafahamu mchango Wao Wakati Mwingine Japo majina Kama Novaty Lufunga na Paul Nonga yameshindwa kuwaokoa 


Pia Gwambina Mmiliki Wao Wakati Ligi ikiwa inaelekea ukingoni aliwahi kunukuliwa akisema kuwa anaamin kufanya kwao vibaya kunachangiwa na Waamuzi kuwaonea Sana na akiamini wanahujumiwa sana Jambo ambalo nadhani halikuwa Sawa Kwa Mmiliki kuja hadharani na kuitaja sababu hiyo pekee kwani kama Makosa ya waaamuzi yamekuwepo sio Tu kwao Ila hata Kwa wengine wengi hapa Siasa ya Mpira iliwatafuna Kucheza huku wakiamini wanaonewa


- MWADUI Hapa Hata Haina Neno Zaidi ya kusema Tu walikuwa Dhoooofu Tangu Siku Za Mwanzo Tu Ligi ikianza kama ilivyokuwa Singida United zile Siku za Mwisho Wakati wakishuka

Post a Comment

0 Comments