NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya kazi ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III kwa Masharti ya kudumu. Tangazo hili ni baada ya kupokea Kibali cha ajira Mbadala chenye Kumb. Na. FA.170/366/01”B”/22 cha tarehe 15 Juni, 2021 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kwa mchanganuo ufuatao:-

Mtendaji wa Kijiji Daraja la III - (NAFASI 1)

i. Sifa za Kitaaluma kwa mwombaji

- Awe amehitimu na kufaulu Elimu ya Kidato cha nne au sita
- Aliyepata mafunzo ya Stadi za kazi ngazi ya Astashahada/Cheti (NTA Level 5) katika fani zifuatazo:-
Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

ii. Mshahara

Kwa kuzingatia Viwango vya serikali atalipwa ngazi ya Mshahara wa TGS B/1 kwa mwezi.

iii. Majukumu ya Mtendaji wa Kijiji

a. Afisa Masululi na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
b. Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji.
c. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya maendeleo ya Kijiji.
d. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kjiji
e. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
f. Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
g. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalum katika Kijiji
h. Kusimamia, kukusanya na kuihifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
i. Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
j. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya Wananchi
k. Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji.
l. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

MASHARTI YA JUMLA YA MUOMBAJI

  •  Awe raia wa Tanzania
  •  Awe na Umri wa Miaka 18-45
  •  Awe hajawahi kufukuzwa kazi, kupunguzwa, kuachishwa na kustaafishwa kazi katika Utumishi wa Umma
  •  Kila mwombaji aambatanishe Wasifu wake (CV), Vyeti vya Shule na Taaluma, Cheti cha kuzaliwa pamoja na picha ndogo 2 (pasport size) zilizopigwa hivi karibuni,
  •  Transcript “Testmonials” na “Provisional Results”au “Statement of Results” havitakubaliwa.
  •  Kila mwombaji aandike kwa usahihi Anwani yake na Namba ya simu inayopatikana muda wote kwa ajili ya mawasiliano
  •  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 27/07/2021
  •  Maombi yote yawasilishwe kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA,
S.L.P 1007,
SINGIDA.

Post a Comment

0 Comments