Taarifa Mpya Kutoka Yanga Kuhusu Kesi ya Morrison.

 


Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) leo imemaliza kulisikiliza kesi ya rufaa ya Klabu ya Yanga dhidi ya Bernard Morrison.

Mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kuanzia sasa mpaka tarehe 24/08/2021.

Uongozi wa Yanga unawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki kuwa na subira, wakati huu ambapo Mahakama hiyo inaendelea kukamilisha uamuzi wake.

Post a Comment

0 Comments