Mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimi anajiandaa kutua Biashara baada ya kumaliza mkataba wake na mabosi wa Yanga kuamua kumkaushia kuuongeza.
Nchimbi alikuwa kwenye kiwango duni msimu ulioisha (2020/21) akiweka rekodi ya kumaliza mwaka mzima pasipo kufunga bao, kutokana na uwezo wake alikuwa anawaniwa na timu tatu ikiwamo Tanzania Prisons, Mbeya Kwanza, na Polisi, lakini Biashara imeonekana kuwa na kisu kikali.
Baada ya klabu ya Al Ahly ya Misri kupeleka ofa kwa klabu ya Simba kumhitaji nyota wao wa kimataifa wa Msumbuji Luis Miquissone. Miamba ya Afrika Kusini Kaizer Chiefs nao wameulizia uwezekano wa kumpata Luis Miquissone. Bodi ya Simba ilisharidhia kumuuza nyota huyo si chini ya dola 650,000 (zaid ya bilioni 1.5 za Kitanzania).
Azam FC wako katika harakati za kukamilisha usajili wa beki wa KMC Andrew Vincent ‘Dante’. Azam inamtaka Dante ili kuziba nafasi ya Yakub Mohammed aliyetemwa na kuunganishwa na wakali wengine walionaswa na matajiri hao kama Edward Charles, Rodgers Kola, Kenneth Muguna na Paul Katema na Charles Zulu.
Kama mambo yakienda vyema, beki wa Biashara United, Abdulmajid Mangalo anaweza akala shavu Simba. Awali ilidaiwa Yanga walikuwa wakimvizia nahodha huyo wa Biashara, lakini wakashindwa na sasa Simba ikitajwa kukaribia kumnasa beki huyo
0 Comments