Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Yusuph Athuman kutoka Biashara United ya Mkoani Mara - Mchezaji huyo kinda aliichezea Mbao FC kabla ya kutua Biashara pia amewahi kusajiliwa na Namungo FC.
Ni zao la Yanga SC kwenye kikosi cha Kina Yusuf Mhilu Mwaka 2015.....Ni kama sasa amerudi nyumbani..
Kiungo wa Kagera Sugar, Abdul Swamadu mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka mitatu kama mchezaji huru. Abdul atatambulishwa muda wowote kuwa mchezaji wa Simba.
Beki wa kulia wa Simba David Kameta Duchu amejiunga na klabu ya Mbeya Kwanza FC kwa mkopo wa msimu mmoja. Duchu mwenye umri wa miaka 20 anaondoka Simba baaada ya klabu hiyo kukamilisha usajili wa beki wa kulia Israel Patrick Mwenda wa KMC.
Winga wa kimataifa wa Malawi na klabu ya Nyasa Big Bullets FC, Peter Banda mwenye umri wa miaka 20 amekamilisha makubaliano na klabu ya Simba muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo kama mbadala wa Luis Miquissone ambaye yupo mbioni kujiunga na Al Ahly ya Misri.
Straika Eliud Ambokile anatajwa kujiandaa kurejea Mbeya City baada ya soka lake la kulipwa nchini DR Congo na Zambia kutokwenda sawa.
Ambokile alijiunga TP Mazembe akitokea City kisha kutimkia Nkana na kote mambo yalienda ovyo na kuamua kurudi nyumbani na sasa mabosi wake wa zamani wanaisaka saini yake.
0 Comments