OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MUONGOZO WA MWANAFUNZI KATIKA MFUMO WA SELFORM
NAMNA YA KUINGIA NA KUBADILISHA MACHAGUO
TOLEO LA KWANZA (Ver 1.0)
(CANDIDATE MANUAL)
Umeandaliwa na:-
Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S.L.P 1923,
DODOMA.
Machi, 2019
JUKUMU LA MWANAFUNZI KATIKA MFUMO WA SELFORM
Mwanafunzi (Muhitimu wa Kidato cha Nne (Form Four)) – Jukumu lake kuu katika mfumo wa Selform ni kubadilisha baadhi ya taarifa binafsi kama Home Address, Mobile Number, Email Address na machaguo ya shule, vyuo na tahsusi zake katika seksheni zingine kutokana na ufaulu katika matokeo yake.
1. NAMNA YA KUINGIA KWENYE MFUMO WA SELFORM
Ukiwa kwenye internet, fungua kivinjari chako (browser mfano, chrome), andika anuani ifuatayo selform.tamisemi.go.tz kupata dirisha la kujaza taarifa zako za kujisajili kama inavyoonekana hapo chini. Bofya Menu ya chini kabisa iliyoandikwa
For Candidates, Click here to Register kama mtumiaji ni mara yake ya kwanza.
Kisha, ujaze taarifa zinazohusika za Index Number kwa format ya Mfano S0101.0020.2018, Jibu swali utakaloulizwa, Jina la Ukoo na Mwaka wa kuzaliwa kama inavyoonekana hapo chini.
Kisha dirisha litafunguka na kutaka ujaze Password utakayoitumia siku zote. Dirisha lifuatalo litafunguka;
Ukishaandika Password, mfumo utaonekana katika sura hii kuonesha umefanikiwa kubadili Password;
Ukishabadili Password, utaitumia kuingia kwa mara nyingine kwa kuandika username mfano S0101.0002.2018 na Password uliyoibadili.
2. PART A: TAARIFA BINAFSI ZA MWANAFUNZI
Ukishaingia kwenye mfumo, dirisha lifuatalo litafunguka na sehemu zilizozungushiwa tu ndio utaweza kubadili taarifa binafsi. Ukimaliza kujaza bofya Save and Next hapo chini ili kuendelea mbele.
0 Comments