BORA KUFUNGWA ILA TUCHUKUE KOMBE


MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa ikiwa ataulizwa kama apoteze mchezo ama atwae taji yeye angechagua kutwaa taji.

Hiyo imetokana na utani wa jadi mwa kuwa walipokutana na Yanga, Julai 3 katika mchezo wa ligi walifungwa bao 1-0 na kuyeyusha pointi tatu muhimu mazima.

Jana, Julai 25 walishinda bao 1-0 mbele ya Yanga katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma .

Ushindi huo unawafanya Simba watetee taji lao la Kombe la Shirikisho ambalo walitwaa msimu uliopita Sumbawanga baada ya kushinda mbele ya Namungo.

Barbara amesema:"Ikiwa ungeniuliza kati ya kufungwa na kuchukua kombe ningependa nini itokee, mimi ningesema bora kufungwa lakini tupate kombe," .


Post a Comment

0 Comments