TANGAZO LA KAZI NGARA DC



 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA

Unapojibu tafadhali taja:

Kumb. Na. EB.89/286/02/19 12/04/2021


YAH: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara anawatangazia nafasi za kazi Wananchi wote wa Tanzania wenye sifa za kuajiriwa kama inavyoonekana hapa chini:-

1. Mtendaji wa Kijiji Daraja la III nafasi 02

2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II nafasi 01


1.1 Sifa za kuajiriwa – Mtendaji wa Kijiji Daraja la III Mwombaji anapaswakuwa na sifa zifuatazo:-

a) Mwenye elimu ya Kidato cha Nne (K.IV) au sita (K.VI).

b) Mhitimu wa Mafunzo ya Astashahada/ Cheti katika moja ya fani za Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, Mipango na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinacho tambuliwa na Serikali.

1.2 Majukumu ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III – Mwombaji atakayefaulu/atakayekidhi vigezo na kuajiriwa atatekeleza majukumu yafuatayo:-

a) Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.

b) Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na Mali zao; na kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.

c) Kuratibu na Kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.

d) Katibu wa Mikutano/Vikao na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.

e) Kutafsiri na Kusimamia Sera, Kanuni, Taratibu na Sheria za Nchi.

f) Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali pamoja na kipato binafsi.

g) Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.

h) Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI>>>>>>>

Post a Comment

0 Comments