Klabu ya Azam imekamilisha utiwaji saini mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco.
Mshambuliaji huyo amesaini mkataba mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya kudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.
Kola anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, kuanzia msimu ujao 2021/2022.
Aidha Kola akiwa Zanaco msimu uliopita, alifunga jumla ya mabao 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia.
0 Comments