TANGAZO LA KAZI WIZARA YA FEDHA NA KALIUA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/L/101 10 Mei, 2021

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya

Fedha na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa

Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mbili (02) kama zilivyoainishwa

katika tangazo hili.

1.0 MWAJIRI: WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NA HALMASHAURI YA WILAYA

YA KALIUA.


1.0.1 MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II - (NAFASI 02)

1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuandika na kutunza Regista zinazohusu shughuli za uhasibu;

ii. Kutunza kumbukumbu za hesabu;

iii. Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na

iv. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

1.0.3 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambuliwa na

Serikali au cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na

hizo zinazotambuliwa na NBAA.


1.0.4 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B.

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za

kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za

maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe

ipasavyo.

iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V)

yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya

wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti

vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na

vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective

boards)

vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati

matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS

SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao

vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na

NACTE).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba

isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko

katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo 

3 yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24, Mei, 2021. Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

S.L.P. 2320 DODOMA.

i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

ii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Limetolewa na; 

KATIBU 

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Post a Comment

0 Comments