Al Ahly Watwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika.

 


Al Ahly ya Misri, imetwaa ubingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuifunga Kaizer Chief ya Afrika Kusini 3-0. 

Kaizer wamecheza pungufu dakika 45 za kipindi cha pili baada ya Happy Mashiane kupewa kadi nyekundi kwa mchezo usiofaa. 

Magoli ya Al Ahly yametupiwa kimiani na Mohamed Sherif dakika ya 53' na Mohamed Afsha mnamo dakika ya  64' na aliyetia msumali wa mwisho ni Amr Al Sulaya katika dakika ya 74' na hivyo ubao kisomeka. Full Time:Kaizer Chiefs 0-3 Al Ahly


Post a Comment

0 Comments