ISHU YA MORRISON CAS BADO NZITO

 


HAJI Mpili, maarufu kama Mzee Mpili ambaye ni mwanachama wa Klabu ya Yanga amesema kuwa laiti kama mchezaji Bernard Morrison angekuwa ndani Yanga angafanya vizuri zaidi tofauti na sasa.

Morrison amekuwa kwenye mvutano mkubwa na Yanga ishu ya mkataba wake ambapo Yanga wamekuwa wakidai kwamba ana dili la miaka miwili na mchezaji anadai kwamba dili lake lilikuwa ni la miezi sita lilikwisha.

Kuhusu hilo ambapo Yanga wameeleza kuwa kesi yake ipo kwenye mahakama ya usuluhishi, (Cas) Mzee Mpili amebainisha kuwa kesi hiyo ni nzito.

Mpili amesema:-“Akili yake waliivuruga na mimi naamini kama angekuwepo Yanga basi angefanya vizuri sana tofauti na sasa, kwa sababu wanasema hayupo kwenye timu ameondoka..

“Ndio maana tumepeleka CAS na kesi yake ni nzito na Morisson mwenyewe alitaka kesi yake iamuliwe hapa na mpira wake umeshapotea.

“Tarehe tatu alionyesha kama shoo tu hakufanya chochote kwani tulizuia mpira wake, na kwenye simu yangu sina namba ya Morisson na siwezi kuongea nae.

Post a Comment

0 Comments