Azam Fc Yatangaza Mwingine, Amesaini Miaka Miwili.

 


Klabu ya Azam FC imetangaza kumsajili beki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama kwa mkataba wa miaka miwili kwa usajili huru akitokea Ruvu Shooting.

"Tunayofuraha kuingia mkataba wa miaka miwili na beki kisiki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama, kwa usajili huru akitokea Ruvu Shooting."


"Mkataba huo utamfanya Manyama kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023."

"Manyama ni mmoja wa mabeki wa kushoto wanaoendelea kufanya vizuri kwenye ligi yetu, ingizo lake ndani ya kikosi chetu ni katika kuimarisha zaidi eneo hilo."

Huo ni usajili wa tatu katika kikosi cha Azam kuelekea msimu ujao, baada ya awali kuwasaini nyota wa kimataifa wa Zambia, kiungo mshambuliaji, Charles Zulu na mshambuliaji, Rodgers Kola.

Post a Comment

0 Comments