Rais wa FIFA ameipongeza Simba ameipongeza timu ya Simba VPL 2020/2021.



Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza timu ya Simba ameipongeza timu ya Simbawa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL ) msimu wa 2020/2021.

Katika barua yake kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Rais Infantino alisema ubingwa ni matokeo ya juhudi na kutekeleza majukumu kwa kila mmoja ndani ya klabu hiyo.

"Naomba uwasilishe pongezi zangu kwa kila mtu aliyehusika katika mafanikio ya Simba SC, na kuwatia moyo waendelee kufanya kazi kwa moyo wa ushirikiano, ari na ushupavu" alisema Rais Infantino katika barua yake.

Pia alimshukuru Rais Karia na TFF kwa kuchangia maendeleo na ustawi wa mpira wa miguu katika ukanda huu na duniani kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments