Afisa Habari wa Simba Haji Manara ameamua kumtolea uvivu Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez.
Haji anadai Mtendaji huyo amekuwa akimuandama sana na kumnyima raha muda wote toka ameshika majukumu hayo.
Kupitia sauti ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao sauti ya mtu anayesadikika kuwa ni Manara imesikika ikisema kwamba miongoni mwa vitu ambavyo vinampa shida ndani ya Simba ni roho ya chuki.
"Barbara una chuki kubwa kwangu, hadi naogopa kula chakula mbele yako. Naacha hii timu kwa ajili yako kwa sababu ya chuki yako kwangu. Unajiona wewe ni Simba kuliko wote, unataka umaarufu kinguvu"
"Nasingiziwa eti nilienda Kigamboni kwenye kambi ya Yanga, vitu hivi ni vya hovyo kabisa. Mimi sinunuliki kwa thamani ya fedha, Barbara kwangu haya ni matusi"
"Barbara amekuwa akinitishia kunifukuza kazi, na kusema Simba sc ni yake yeye na Mo. Nimefanya kazi muda mrefu bila mkataba kwa kulipwa mshahara wa laki saba"
"Nimetengeneza imani kubwa kwa mashabiki wa Simba, namuhakikishia Barbara atakuwa wa kwanza kuondoka Simba kabla yangu"
"Unadharirisha wafanyakazi, kwa nini, Dkt. Kashembe umemfukuza kazi,unashida gani ? Shida yako umaarufu ? Unenitumikisha kwa muda gani bila kunilipa ? Mimi niende Kigamboni niihujumu Simba ? Haiwezekani hata kwa pesa yoyote ile"
"Unatamba wewe ndio mwenye timu na Mo, sawa. Tutawaambia mashabiki na naituma hii crip mashabiki wajue. We unaijua Simba ! toka wapi wewe ? Nimewekeza jasho langu hapa Simba miaka mingi lakini leo hii useme nilikuwa Kigamboni! Lini nimeenda Kigamboni mimi ?!
Haji Manara
Afisa Habari wa Simba
0 Comments