KUITWA KAZINI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

 


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wanane (8) wa nafasi mbalimbali Serikalini ambao wametajwa majina yao katika tangazo hili wafahamu kuwa walifaulu usaili na kuhifadhiwa katika kanzidata (Database). 

Hivyo, kufuatia kufaulu kwao usaili na kupatikana kwa nafasi wazi zinazohitajika kujazwa, wamepangiwa kituo cha kazi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazijachukuliwa na Wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.

Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

news TANGAZO LA KUITWA KAZINI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI 

Post a Comment

0 Comments