Luis Miquissone Huyoo Misri



 Al Ahly ya Misri imeripotiwa kufikia makubaliano na Simba SC kumsajili kiungo wao nyota Luis Miquissone katika dirisha la usajili la sasa - Miquissone amekuwa akihusishwa na Al Ahly kwa miezi kadhaa sasa, haswa baada ya kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ubora wa hali ya juu, ambapo alifunga bao la ushindi dhidi ya mabingwa hao wa Afrika katika hatua ya makundi.


Ahly wameendelea kuimarisha eneo lao la ushambuliaji msimu huu na wamemfanya Miquissone kama mmoja wa wataosajiliwa msimu huu pamoja na Soufiane Rahimi wa Raja Casablanca....Kulingana na vyanzo nchini Misri, Ahly imewasiliana na Simba na wamefikia makubaliano ya awali kwa mchezaji huyo wa miaka 26 na sasa wataanza mazungumzo na mchezaji huyo na wawakilishi wake kuzungumzia juu ya mkataba wake.


Kocha mkuu wa Ahly, Pitso Mosimane anamjua Miquissone vizuri kwani hapo awali alimfundisha huko Mamelodi Sundowns... Miquissone alijiunga na Sundowns mnamo Januari 2018, lakini alipelekwa kwa mkopo huko Chippa United, Royal Eagles FC, na UD Songo, kabla ya kujiunga na Simba mnamo Januari 2020 - Tangu ajiunge na Simba, Miquissone amekuwa ndani ya ligi kuu Tanzania Bara, Pia akifunga mabao matatu na Assists tatu katika msimu huu ya Ligi ya Mabingwa, ambapo walifika robo fainali.


Post a Comment

0 Comments