Masau Bwire Kuhusu Tukio la Morrison



Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Ruvu Shooting Masau Bwire amejitosa kwenye mjadala wa tukio la kuvua nguo lililofanywa na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison, baada ya timu yake Simba SC kutwaa ubingwa wa Kombe Shirikisho ‘ASFC’ Jumapili (Julai 25) mkoani Kigoma.

Morrison alivua bukta na kuivaa kichwani huku akibaki na nguo ya ndani na kukimbia katika eneo la kuchezea la Uwanja wa Lake Tanganyika akiwa anashangilia Ubingwa wa Kombe la Shirikisho baada ya Simba SC kuifunga Young Africans bao 1-0.

Masau Bwire ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii: “Nadhani ni utovu wa nidhamu, ndiyo maana baadhi ya viongozi wake, wanamlazimisha kuvaa nguo!”

“Au ninyi wadau wenzangu mnasemaje?”

Mwingine alieingia kwenye mjadala huo ni Mwalimu Kashasha ambapo amesema kiungo wa Simba SC Bernard Morrison amekuwa akifanya matukio ya ajabu sana tangu atue Tanzania.

Mwalimu Kashasha amesema: “Simba wanakila sababu ya kumfanyia check ya ubongo (akili) maana matukio anayofanya kwenye soka letu ni mageni kabisa na ya kudhalilisha kabisa.”

Post a Comment

0 Comments