Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji “Mo Dewji” amesema kuwa hakuna mtu mkubwa zaidi kuliko klabu hiyo na wote waliopo waliikuta na wataiacha akiwemo yeye.
"Hata mimi ni mdogo kuliko Simba, wote tumezaliwa tunaikuta klabu hii na tutaiacha na wengine watashika nyadhifa tofauti ndani yake,” amesema Mo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Simba kuachana na aliyekuwa msemaji wao, Haji Manara.
0 Comments