Dondoo Za Soka na Tetesi za Usajili Tanzania Bara leo 31.07.2021



📝Wakala wa mshambuliaji Medie Kagere, Patrick Gakumba amesema taarifa za mchezaji huyo kuwa amewasilisha barua ya kuachana na Simba SC si za kweli. 

Gakumba ameeleza kuwa Kagere amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simba ambapo mkataba huo kwa sasa ni kificho, hawajauweka wazi.

📝Inasemekana kuwa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda,Emmanuel Okwi mwenye Umri wa Miaka 28 ameshamalizana kila kitu kwa mazungumzo na uongozi wa Klabu ya Simba na kilichosalia ni kusaini mkataba na kutambulishwa.

✅𝗗𝗘𝗔𝗟 𝗗𝗢𝗡𝗘 Aliyewahi kuwa mlinda mlango wa Tanzania Prisons Sports club,, Hassan Msham asaini kandarasi tena kukipiga Tanzania prisons.

✅Beki wa kushoto wa Tanzania Prisons U20, Ibrahim Abdallah Abraham amepandishwa kuichezea  Timu kubwa.

✅Athanas Mdam amesaini kandarasi ya kuitumikia Tanzania prisons kwa misimu miwili 2021-2023.

🗣️Bumbuli:Yanga yamrejesha Juma Mahadhi

“Mahadhi amerejea rasmi katika klabu yake aliyokuwa anaichezea akitokea Ihefu tulipompeleka kwa mkopo wa miezi sita pekee.

“Hivyo Mahadhi ataungana na wachezaji wengine watakaokuwepo kwenye kikosi chetu kitakachoshiriki michuano ya Kagame.”

📝Timu ya Tanzania yatwaa ubingwa wa CECAFA U23 kwa mikwaju ya penati 6-5 dhidi ya Burundi kwenye mchezo wa fainali

FT' Tanzania 0-0 Burundi (Pen: 6-5)

📝Beki wa klabu ya Yanga Lamine Moro na mshambuliaji Michael Sarpong wote raia wa Ghana wameondoka nchini (Tanzania) kuelekea kwao Ghana. Moro anaondoka baada ya kusitisha mkataba wake na klabu ya Yanga. 

Mshambuliaji Sarpong wameshindwana na Yanga kuvunja mkataba wake. klabu ya Yanga ilikuwa tayari kuvunja mkataba kwa kumlipa mshahara wa miezi miwili huku Sarpong akitaka milioni 77 ili kuvunja mkataba.


📝Kikosi cha Yanga kitakacho shiriki mashindano ya Ceacafa Kagame CuP kimeshaingia Kambini tayari kwa mashindano.

📝Kiungo wa klabu ya Yanga Sc Mukoko Tonombe amefungiwa mechi tatu na shirikisho la soka la Tanzania TFF pamoja na faini ya Tsh. Laki tano (500,000/-) kwa kosa la kumpiga nahodha wa klabu ya Simba Sc John Bocco wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam Sports Julai 25 katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma

📝Nyota wa Simba Bernad Morrison kiungo wa Simba SC amefungiwa michezo mitatu na faini ya Tsh 3,000,000 kwa kosa la kimaadili alilolionesha siku ya fainali ya ASFC kati yao Simba SC na Yanga SC .

📝Mchezaji wa kimataifa wa DR Congo, Fiston Mayele amethibitisha kuwa atatua nchini Jumapili.

Wakati huohuo, beki wa kulia, Shabani Djuma, amekiri kuwa yeye atachelewa kutua nchini ambapo atatua Agosti 4 akitokea nchini DR Congo.

Post a Comment

0 Comments