TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kupitia Kibali cha Ajira Mbadala kwa Watendaji wa Vijiji, Kibali chenye Kumb. Na. FA 170/358/01’’C’’/48 cha tarehe 24 Mei,2021 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais. Mkurugenzi Mtendaji anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kuomba kazi ili kujaza nafasi za kazi ya AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III.
1.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III - NAFASI 01
1.1SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na cheti cha kufaulu Kidato cha Nne (IV) na waliohitimu mafunzo ya Cheti (Astashahada) katika fani zifuatazo: Utawala, Uongozi na Usimamizi wa Fedha, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
1.2 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
ii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka zaKijiji.
iii. Kiongozi wa wataalam (watumishi wa serikali) katika kijiji.
iv. Mhasibu (Afisa masuuli) na Mtendaji Mkuu wa kazi za kila siku za Serikali ya Kijiji.
v. Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Taratibu zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
vi. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
vii. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
viii. Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
ix. Kutekeleza shughuli nyingine atakazopangiwa na Mwajiri.
x. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
v. Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, Hati Matokeo za Kidato cha Nne na Sita, yaani FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS HAVITAKUBALIWA.
vii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 26 Julai, 2021 saa 9:30 Alasiri.
viii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili fasaha au Kiingereza fasaha na yatumwe kupitia Posta kwa anuani ifuatayo:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO,
S.L.P 43,
KIBONDO
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KIBONDO 14-07-2021
0 Comments