Rasmi Mo Dewji atia mzigo wa Bilioni 20 Simba

 



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji amekabidhi kitita cha Sh 20 Bilioni ambazo ni asilimia 49 ya hisa ambazo anapewa mwekezaji katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.

Dewji amekabidhi cheki ya pesa hiyo leo Julai 30, 2021 huku akieleza kwamba pesa aliyoiweka Simba ni zaidi ya Bilioni 20.

"Mpaka sasa nimeshaipa Simba Sh 21.3 Bilioni, ukiachana na pesa nyingine za ziada za maandalizi ya msimu, usajili na nyinginezo ninazotoa,"

Lakini kuna watu wanasema Mohammed Dewji hana pesa, leo hii nakabidhi cheki ya Sh 20 Bilioni za hisa asilimia 49 kwa klabu ya Simba," amesema.

Alitania kwamba kama angesema pesa hiyo Bilioni 20 tayari ameshaipa Simba na wamemalizana kwenye zile Bilioni 21.3 alizokwishazitoa Simba kwa miaka minne iliyopita ingekuwa ni sawa.

Nimewekeza kwa damu, jasho, na machozi ndani ya Simba. Simba ni kubwa kuliko mimi, ni kubwa kuliko kila mtu. Sisi ni Simba. Nawashukuru Wanasimba na Watanzania. Nisingekua hapa bila ya nyie wote. Tupo pamoja

Post a Comment

0 Comments