TANZANIA, BURUNDI CECAFA U23 FAINALI LEO
Fainali ya michuano ya kombe la Cecafa kwa vijana chini ya umri wa miaka 23, inatarajiwa kuchezwa leo kati ya Tanzania na Burundi.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Bahir Dar nchini Ethiopia kunakofanyika michuano hiyo.
Mara ya mwisho Tanzania kuchukua kombe hilo ni mwaka 2010 huku Burundi ikiwa haijawahi kuchukua zaidi ya kuishia nafasi ya pili mwaka 2013.
0 Comments