Rayvanny amesafiri kwenda Zimbabwe ambako anatarajiwa kufanya kazi kwenye mradi wa muziki na msanii anayefahamika kama Rockford 'Roki' Josphats.
Ripoti zinaonyesha kuwa Rayvanny atakuwa akifanya kazi ya remix kwa moja ya nyimbo za Rockford ambayo bado haijajulikana.
Rockford 'Roki' Josphats ni miongoni mwa wanamuziki wanaotamba sana katika tasnia ya Burudani ya Zimbabwe. Amesainiwa chini ya lebo ya rekodi ya Passion Java ambayo inamilikiwa na Prophet Passion Java.
Prophet Passion Java ni rafiki wa karibu wa Rayvanny na anaonekana ndiye aliyesababisha safari ya Rayvanny kwenda Zimbambwe. Passion Java alikuwepo wakati wa uzinduzi rasmi wa lebo ya rekodi ya Next Level ambayo inamilikiwa na Rayvanny.
Wakati wa uzinduzi, alitambulishwa kama rafiki wa karibu wa Rayvanny. Kwa upande mwingine, Rayvanny amekaa kimya kuhusu ziara yake Harare na bado hajafafanua maelezo ya wimbo ambao watafanya remix.
Hii inakuja muda mfupi tu baada ya Rayvanny kumaliza ushirikiano wake na mwanamuziki wa Nigeria Guchi kwenye wimbo wa ‘Jennifer Remix’.
Jennifer Remix imepokelewa vizuri na imepata watazamaji wengi ndani ya muda mfupi. Inaonekana kuwa idadi nzuri ya wanamuziki wa Kitanzania wanafanya kazi ya remix kwa nyimbo mbali mbali. Wanamuziki wengine ambao pia wametangaza kuwa wanaandaa remix ni Anjella na Harmonize
0 Comments