Shangazi ateuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba akichukua nafasi ya Barbara Gonzalez




MBUNGE wa Jimbo la Mlalo, Rashid Abdallah Shangazi ambaye ni Mwenyekiti wa Tawi la Simba Bungeni maarufu 'Wekundu wa Mjengoni' ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba akichukua nafasi ya Barbara Gonzalez, aliyeteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu.
Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika medani za kiuongozi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisiasa, Rashid Abdallah Shangazi kwa sasa si tu Mbunge anayewakilisha Jimbo la Mlalo mkoani Tanga bali pia ni Kamishna wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni Katibu wa Wabunge wanaowakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) na Mwenyekiti wa Wananchama wa Klabu ya Simba Tawi la Bungeni maarufu Wekundu wa Mjengoni.

Shangazi ni mtu anayeamini katika kufanya kazi kwa umoja na kuongoza umma kwa nguvu ili kuleta mafanikio chanya na haogopi kuchukua hatua yoyote.
Lakini pia Rashid ana uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea katika mazingira ya mabadiliko na changamoto kwenye muda uliowekwa na vipaumbele.
Ana ujuzi mzuri wa masuala ya Uendeshaji wa Biashara na mwenye shauku ya kusaidia makundi mbalimbali katika jamii ili kufikia malengo yao.
Kama mtu aliyefanikiwa na ambaye ana rekodi nzuri ya utoaji na malengo yaliyozidi anaweza kutegemewa kupunguza gharama zote zisizohitajika katika mazingira yoyote na kufikia malengo. Yeye ni mtu bora anayetamani kutoa ubora katika kila fursa.



Post a Comment

0 Comments