Soma Hii Kuhusu Mkataba wa Morrison na Yanga.



FIFA Transfer Matching System (TMS) inafanya kazi mara moja tu kila muda wa usajili unapofunguliwa na kufungwa basi, hii ina maana kubwa sana katika kulinda usahihi kwa mchezaji toka sehemu moja kwenda nyingine. 

Morrison msimu wa 2019/2020 (January 2020) alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miezi sita na ndio uliowekwa kwenye TMS hapa ina maana system ilifungwa mpaka dirisha kubwa la June 2020.

Mkataba wa extension wa Morrison na Yanga ambao ndio unaleta ukakasi na kesi iliyopo CAS haukuwepo kwenye system (TMS) sababu ulifanyika system ilishafungwa, ulikuwa unasubiria mpaka system iwe wazi tena ili uingizwe. 

Baada ya hukumu ya kamati ya hadhi za wachezaji mwezi wa sita (June) Morrison aliweza kuwa huru na kusajiliwa na Simba kwasababu System ilionyesha hivyo kutokana na mkataba uliokuwepo ni ule wa miezi 6 na sio huo mpya wa miaka miwili.

Simba waliweza msajili Morrison akiwa huru na TMS ilikubali ombi la Simba kuweka data zake kutokana na ukweli huo, kama ingekuwa ule mkataba wa Extension wa Yanga upo kwenye TMS basi Simba walipaswa kuomba kwa Yanga Release letter ya mchezaji au kufanya Transfer (kutoka Yanga kwenda Simba) ambalo ingekuwa gumu sana kukubaliwa na Yanga.

Kwa Mantiki hiyo suala la Case iliyopo sasa CAS haiwezi kuadhiri chochote msimu wa 2020/2021 kwenye matokeo katika mkataba wa Morrison na Simba ulikubalika kwa TMS, hata hivyo Yanga hawajawahi kuweka pingamizi kuhusu usajili huo popote pale pindi tu Morisson alipotangazwa kuwa mchezaji wa Simba msimu huu.

Iwapo Yanga ikishinda atakayeadhibiwa ni Morisson na Morisson akishinda itakayoadhibiwa ni Yanga.

Post a Comment

0 Comments