Huyu Hapa Mrithi Wa Luis Miquissone Simba.

 

WINGA machachari wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda ameweka wazi kuwa yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Simba huku mwenyewe akiweka wazi kuwa tayari kuitumikia klabu hiyo.

Simba imeonyesha nia ya kumhitaji winga huyo tangu alipoonyesha kiwango bora katika mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Malawi uliofanyika Juni ambapo Tanzania iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar. 

Akizungumzia dili hilo, Winga huyo amesema kuwa yupo katika mazungumzo na uongozi wa Simba ambao nwameonyesha nia ya kumhitaji huku mwenyewe akiweka wazi kuwa yupo tayari kujiunga na klabu hiyo kama watakamilisha taratibu zote za usajili.

“Simba walinitafuta kabla hata sijacheza katika mchezo wa kirafiki pale Tanzania, lakini baada ya kuja kucheza huko ndipo walipoongeza nguvu katika masuala yao ya usajili, mpaka sasa hakuna ambacho kimekamilika kuhusu usajili wa kujiunga nao.

“Kama akitokea wamekamilisha basi sina tatizo kujiunga na Simba, ni timu kubwa na inafanya vizuri Afrika, ukizingatia kuhusu uhamisho ndio hutokea mara zote kwa wachezaji kwa kuwa ndio ajira yetu,” amesema winga huyo.

Kama simba itakamilisha usajili wa winga huyo ambaye anacheza katika nafasi moja na Luis ni wazi kuwa ataenda kuziba pengo la Luis Miquissone ambaye anaweza kutimkia katika klabu ya Al Ahly ambao wameonyesha nia kubwa ya kumhitaji

Post a Comment

0 Comments