Tofauti ni presha ya kupoteza mechi iliyopo Simba sio kama ile ya Azam.



Mshambuliaji wa klabu ya Simba John Raphael Bocco akizungumza kwenye kipindi cha Michezo cha Cloudsfm, "SportsExtra" amefunguka utofauti uliopo kwenye timu yake ya sasa na timu aliyokua akiitumikia mwanzo ya Azam FC.

"Ukiangalia timu yetu ya msimu huu na misimu miwili iliyopita ni tofauti, kila msimu timu inazidi kuwa imara. Maingizo mapya na maboresho ya kila msimu yanakuwa msaada mkubwa kwenye timu. Hicho ndio kitu kikubwa kinachotusaidia kuwa bora kwa kila msimu."


"Nilipokuwa Azam FC story nilizokuwa nasimuliwa kuhusu Simba ni tofauti kabisa na mambo niliyoyakuta. Niliambiwa kuhusu changamoto nyingi lakini tangu nimefika Simba zile changamoto nilizokuwa nazisikia sijakutananazo.


Tofauti kubwa ni presha ya kupoteza mechi iliyopo Simba sio kama ile ya Azam."

Aidha amezungumzia kiufupi maisha ya washambuliaji pacha wake Medie Kagere na Mugalu.

"Kagere na Mugalu ni watu safi sana. Hata kwa maisha ya kawaida tunaishi vizuri sana, hata ndani ya uwanja ushirikiano wetu ni mkubwa sana.


Mimi binafsi nafurahia kuwanao, wananipa ushirikiano kwa 100% na mimi nawapa ushirikiano. Ni wachezaji wazuri na kila mmoja kwa wakati wake anaisaidia timu."


- John Bocco on SportsXtra cloudsfm



Post a Comment

0 Comments