Kocha wa zamani wa Harambee Stars Sebastien Migné ameteuliwa kuwa kocha wa Klabu ya Mallamo Gallants baada ya timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini kuachana na Dylan Kerr mapema wiki hii.
Kerr ambaye pia alifundisha Gor Mahia ya Kenya inasemekana alikataa kuongeza mkataba wake.
Migné aliiongoza Kenya kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2019 nchini Misri, ambayo ni ya kwanza tangu 2004, na hapo awali aliwahi kufundisha timu za taifa za Equatorial Guinea na Kongo pia.
0 Comments