JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA.
Kumb. Na. EA.7/96/01/L/33 16 Februari, 2021
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji
kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 08 – 30 Januari, 2021 kuwa
matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa
katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia imejumuisha baadhi ya wasailiwa
waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao
wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha
kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo
katika majengo ya Asha Rose Migiro yaliyomo ndani ya Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya
tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika
zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa
kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za
kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za
masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya
kupewa barua ya Ajira isipokuwa wale tu waliopangiwa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) utaratibu wao wa kuripoti umeainishwa katika aya inayofuata.
Waombaji kazi wote waliopangiwa kituo cha kazi Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) wanatakiwa kuripoti tarehe 25 Februari, 2021 saa 2:00 asubuhi katika
ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi tayari kwa kuelekea katika
kambi ya mafunzo ya Jeshi Usu. Sambamba na vyeti halisi waombaji hao
waliofaulu watatakiwa kuwa na vifaa vifuatavyo vya lazima; nguo ya mazoezi
(Track Suit), Raba, Fulana, Bukta, Begi la mgongoni (Day Pack/Rucksack) na
Soksi jozi za kutosha.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa
hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine
nafasi za kazi zitakapotangazwa.
0 Comments