UTANGULIZI
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (Sayansi miaka mitatu). Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha NNE wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (sayansi miaka mitatu) ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III.
AINA YA MAFUNZO NA SIFA
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo
A. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA AASTASHAHADA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI
Na. | AINA YA MAFUNZO | SIFA ZA KUJIUNGA | VYUO | MUDA WA MAFUNZO |
1. | Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi |
| Bustani TC, Ilonga TC, Kabanga TC, Katoke TC Kitangali TC, Kinampanda TC, Mandaka TC Mtwara (U) TC, Mhonda TC, Murutunguru TC Mpuguso TC, Singachini TC, Tandala TC, Tarime TC Vikindu TC, Nachingwea TC, Ndala TC, Mamire TC, Shinyanga TC, Marangu TC,Tabora TC, MonduliTC na Dakawa TC | Miaka 2 |
2. | Astashahada ya Ualimu Elimu Maalum |
| Patandi TC | Miaka 2 |
3. | Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali |
| Kinampanda TC, Nachingwea TC, Mhonda TC Tarime TC, Vikindu TC, Mpuguso TC, Mandaka TC, Singachini TC Murutunguru TC, Kabanga TC, Bustani TC Ndala TC, Katoke TC, Bunda TC, Tarime TC | Miaka 2 |
4. | Astashahada ya Ualimu Elimu kwa Michezo |
| Tarime TC, Mtwara (K) TC, Ilonga TC | Miaka 2 |
5. | Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (English Medium) |
| Dakawa TC, Marangu TC | Miaka 2 |
B. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI (SAYANSI)
Na. | AINA YA MAFUNZO | SIFA ZA KUJIUNGA | VYUO | MUDA WA MAFUNZO |
1. | Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati | Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III kwa masomo ya: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agriculture Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science. | Monduli TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC na Tabora TC | Miaka 3 |
C. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (ASTASHAHADA ELIMU MSINGI ELIMU MAALUMU)
Na. | AINA YA MAFUNZO | SIFA ZA KUJIUNGA | VYUO | MUDA WA MAFUNZO |
1. | Astashahada Elimu Maalum (Mafunzo kazini) Msingi | Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Astashahada, Stashahada au Shahada kwa ufaulu wa angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Nne na awe na uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka miwili (2) | Patandi TC | Miaka 2 |
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
- Wahitimu wa kidato cha nne waliohitimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 wanaruhusiwa kutuma maombi.
- Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kielektroniki kupitia tovuti (tcm.moe.go.tz)
- Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki.
- Waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali watachagua tahasusi hadi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi
- Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada au Shahada.
- Walimu Kazini watapaswa kuambatisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao;
- Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia 15/06/2021 ) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.
- Barua na fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
- Mwisho wa kutuma maombi kwa Mafunzo ya Ualimu ni tarehe 31/05/2021.
Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.
Kwa mawasiliano zaidi piga 0620198019. Namba hiyo inatumika siku za kazi (Jumatatu hadi Ijumaa) muda wa kazi 1.30 asubuhi hadi 9.30 alasiri.
IMETOLEWA NA KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
0 Comments