📝Beki wa kushoto Brayson David atakuwa miongoni mwa wachezaji wapya ambao wataichezea klabu ya Yanga kwenye mashindano ya Kagame Cup ambayo yanatarajia kuanza Jumapili ya August 01.
📝Klabu ya Yanga imeweka wazi kuwa haimuuzi kiungo wao fundi Feisal Salum,kwani yuko kwenye project yao.
Hii ni baada ya Klabu ya Tp Mazembe ilihitaji huduma ya kiungo Huyo mwenye umri wa miaka (23) Feisal Salum anamkataba wa miaka mitatu na klabu yake ya Yanga hadi (2024)
📝Golikipa wa Klabu ya Aiggle Noir ya Burundi Eric Johora raia wa Tanzania atakuwa miongoni mwa wachezaji ambao wataichezea klabu ya kwenye michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza August 1,2021 Jijini Dar.
Johora bado hajasiani mkataba na Yanga iwapo ataonesha kiwango kizuri atasajiliwa moja kwa moja huku Beki wa kushoto wa KMC Brayson David na Winga wa Dodoma Jiji Dickson Ambundo wao walishasajiliwa tayari na klabu ya Yanga.
📝Kaa tayari kwa mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji na wanahabari ambao utafanyika leo kuanzia saa 5:00 asubuhi.
📝Kaimu mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya klabu ya Simba Ezekiel Kamwanga Leo ameanza kazi rasmi baada ya kuteuiwa na Bodi ya wakurungezi ya Simba kukaimu nafasi iliyoachwa na Haji Manara kwa muda wa miezi miwili.
📝Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) leo imemaliza kulisikiliza kesi ya rufaa ya Klabu ya Yanga dhidi ya Bernard Morrison.
Mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kuanzia sasa mpaka tarehe 24/08/2021.
Uongozi wa Yanga unawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki kuwa na subira, wakati huu ambapo Mahakama hiyo inaendelea kukamilisha uamuzi wake.
📝Uongozi wa klabu ya Yanga imetangaza kuachana na meneja wa media za klabu hiyo Dismas Ten baada ya mkataba kuisha. Uongozi wa Yanga unamtakiwa kila la kheri katika maisha yake nje ya Yanga. Ten alijiunga na Yanga July 2017 kama afisa Habari akitokea Mbeya City na akiwa Yanga amewahi kuwa Afisa Habari, Kaimu katibu mkuu, Meneja wa Timu, Afisa masoko na Sasa anaondoka akiwa Meneja wa Media za Yanga.
0 Comments