Dondoo Mbalimbali Za Soka Afrika leo 28.07.2021

 


➖Bernard Morrison amekabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Juni (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month). 


➖Mdhamini mkuu kampuni ya SportPesa metukabidhi Tsh. 100 milioni kwa klabu ya Simba kama zawadi baada ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu 2020/21.

➖Taarifa za kuaminika kutoka Morocco zinaeleza kuwa klabu FAR Rabat inayonolewa na kocha Sven imekuwa na mazungumzo na Simba kuhusu huduma Miquissone na Chama. Mpaka sasa hakuna ofa rasmi iliyotumwa kwa ajili ya Chama. Maofisa wa FAR Rabat wanasema ada za uhamisho kwa wachezaji hao ni kubwa mno

➖Shirikisho la mpira wa miguu nchini Uganda "FUFA" limemtangaza Milutin Sredojević raia wa Serbia kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes' Micho aliwahi kuifundisha The Cranes mwaka 2013-2017.

➖Makundi ya Kagame Cup 

Kundi A

1-KCCA (Uganda)

2-Le Messanger Ngozi FC (Burundi) 

3-KMKM (Zanzibar)

Kundi B 

1-Azam FC (Tanzania)

2-Tusker FC (Kenya)

3-Atlabara FC (Sudan Kusini) 

Kundi C 

1-Yanga SC (Tanzania) 

2-Express FC (Uganda)

3-Nyassa Big Bullets (Malawi)

➖Mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo Ben Malango Ngita amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Al Sharjah SC ya Falme za kiarabu (UAE) akitokea Raja Casablanca ya Morocco kwa dau la dola milioni 3.5 (Zaidi ya Bilioni 8.1 za Kitanzania).

➖Klabu ya Cape Town City imevunja mkataba na mshambuliaji Justin Shonga raia wa Zambia. Shonga (24) alijiunga na klabu hiyo January 2021 akitokea klabu ya Tshakhuma Tsha Madzivhandila FC na kusaini mkataba wa miaka mitatu. Akiwa Cape Town City alicheza mechi 13 bila kufunga goli pia Shonga amewahi kucheza Orlando Pirates ambayo aliachana nayo September 2020 na kujiunga Tshakhuma.

➖Klabu ya Power Dynamos ya Zambia imekamilisha usajili wa kiungo Tiki Chiluba kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Indeni FC ya Zambia.

➖Klabu ya Zamalek SC inamtaka kiungo wa kimataifa wa Venezuela na klabu ya Caracas FC, Edson Daniel Castillo Garcia kuwa mbadala wa kiungo Ferjani Sassi ambaye amejiunga na Al-Duhali ya Qatar. Castillo mwenye umri wa miaka 27 alicheza mechi 4 za Copa America 2021 akafunga goli 1 na kutoa assist 1.

➖CAF imemfungia mwaka mmoja kucheza soka nahodha wa Enyimba Augustine Oladapo baada ya kubainika kuwa alitumia dawa zisizoruhusiwa michezoni, Augustine alipimwa mwezi May 2021 baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC ya Misri.

➖TANZANIA HAOOOOOOO FAINALI

Hatimaye majemedari wamefanya kazi yao ya kuiheshimisha nchi kwa kuwalaza wanubi na kutinga fainali

Post a Comment

0 Comments