Klabu ya Geita Gold FC ambayo itashiriki ligi kuu ya Vodacom (VPL) kwa msimu wa 2021/22 imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Mwadui FC na KMC FC, Salim Ayee kwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu ya Azam FC imefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wao wanne wa kimataifa. Wachezaji hao ni beki wa kati, Yakubu Mohammed (Ghana), kiungo Ally Niyonzima (Rwanda), mshambuliaji Mpiana Monzinzi (DR Congo) na Obrey Chirwa (Zambia) ambaye mkataba wake umemalizika.
Mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo na klabu ya Wydad AC ya Morocco, Francy Kazadi Kasengu ambaye alikuwa anacheza Al-Masry ya Misri kwa mkopo yupo katika hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya Yanga ya Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja. Kazadi mwenye umri wa miaka 29 ana thamani ya Euro 250,000 (zaidi ya milioni 680 za Kitanzania).
Mitandao ya nchini Misri imeripoti kuwa klabu ya Al Ahly tayari imefikia makubaliano na klabu ya Simba juu ya uhamisho wa mshambuliaji wao Luis Miquissone raia wa Msumbuji. Simba tayari imeridhia kuumuza nyota huyo kwa dau la dola 560,600 (bilioni 1.3 za Kitanzania). Pia Al Ahly inaweza ikamtoa mshambuliaji wao Walter Bwalya kwenda Simba.
KLABU ya Simba inaripotiwa kuwa wapo Serious na mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji kinda wa kimataifa wa Malawi, Peter Band anayekipiga kwa mkopo ndani ya klabu ya Sheriff Tiraspol akitokea klabu ya Nyasa Big Bullets.
0 Comments