Tetesi za Usajili Simba leo July 24.2021

 


KLABU ya Simba inaripotiwa kuwa wapo Serious na mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji kinda wa kimataifa wa Malawi, Peter Band anayekipiga kwa mkopo ndani ya klabu ya Sheriff Tiraspol akitokea klabu ya Nyasa Big Bullets.

Imeelezwa kuwa Simba inataka kumuongeza Banda mwenye umri wa miaka 20, kama mbadala wa Mzimbabwe, Perfect Chikwende ambaye ameonekana kupata wakati mgumu kuendana na utamaduni wa Simba kiasi cha kuondolewa kikosini, huku taarifa zikieleza kuwa huenda Simba ikaachana naye au kumtoa kwa mkopo mwishoni mwa msimu huu.

Hivi karibuni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Zacharia Hanspope alifunga safari na kwenda nchini Malawi, huku ikielezwa kuwa miongoni mwa usajili wa wachezaji ambao alikuwa amekwenda kumalizana nao ni ule wa Banda

Post a Comment

0 Comments