KAMBI YA SIMBA ITAKUA NCHI HII HAPA



Mara baada ya Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara, Simba  kuthibitisha kutoshiriki mashindano ya Kombe la Kagame na kuwapa mapumziko ya siku 10 wachezaji wake. Imeelezwa kuwa klabu hiyo itaweka kambi yake kunako viunga vya nchi ya misri.


Inaelezwa kuwa mabingwa hao watarejea kambini na kuondoka kwenda nchini Misri Agosti 8 kuweka kambi mpaka Agosti 28.


Wakiwa nchini Misri mabingwa hao mara nne mfululizo wa Ligi Kuu watacheza mechi za kirafiki kwa ajili ya utimamu wa miili ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu.

Post a Comment

0 Comments