Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Michael Sarpong raia wa Ghana ameuambia uongozi wa klabu ya Yanga kuwa kama wanataka kuvunja mkataba wake uliobaki lazima wamlipe dola 31,000 (zaidi ya milioni 71 za Kitanzania) za kuvunja mkataba wake na si vinginevyo.
Sarpong mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Yanga August 2020 kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru baada ya kuachana na Rayon Sports ya Rwanda kwa sasa nyota huyo hayupo kwenye mipango ya msimu ujao ya kocha Nabi na ameambiwa nia ya klabu hiyo ya kuvunja mkataba wake.
0 Comments