Lamine avunjiwa mkataba Yanga



Yanga kiroho safi jana Jumatano imeachana na aliyekuwa nahodha wao, beki Lamine Moro. Uongozi wa klabu hiyo umefikia uamuzi wa kuachana na Moro ambaye ameitumikia Yanga kwa mwaka mmoja na nusu huku akiwa mkali wa mabao ya vichwa.

Hatua ya kusitisha mkataba wa beki huyo hautokani na kiwango chake, bali inaelezwa kuwa kitendo cha Lamine kutofautiana na kocha wa timu hiyo, Nesreddine Nabi pamoja na kuyumba kwa nidhamu yake hivi karibuni ndio kimepelekea kuvunjiwa mkataba.

Inaelezwa katika makubaliano hayo Yanga na Moro wamekubaliana watalipana mshahara wa mwezi mmoja.

Post a Comment

0 Comments