Mshambuliaji kutoka nchini Burundi na Klabu ya Young Africans, Saido Ntibazonkiza, amesema hataachana na klabu hiyo kama taarifa za mitandaoni zilivyoibuliwa jana Jumapili (Julai 18).
Ntibazonkiza amesema bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Young Africans, na wanaliomzulia ataondoka klabuni hapo ni ‘WAONGO’.
Amesema wazushi wa taarifa hizo wamekua wakiibua taarifa tofauti tofauti mbali na yeye kuondoka Young Africans, ili kuifanya mitandao ya kijamii kuwa sehemu za starehe na kuwaburudisha wanaowafuatilia.
Ilidaiwa kuwa Ntibazonkia aliandika ujumbe wenye utata kwenye urasa wake wa mtandao ya kijamii wa Instagram, baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji FC uliomalizika kwa sare ya bila kufungana, Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Jana Jumapili (Julai 18).
Mshambuliaji huyo aliandika: Huenda ukawa wa mwisho kwangu….. Lakini sio mwisho, Mungu pekee ndio anajua.
Baadae Haruma Niyonzima alimjibu kwa kuandika: Ninaamini kila kitu kitakua sawa kaka yangu ‘In Shaa Allah
0 Comments