MAKAMBO AAGWA RASMI HOROYA, DILI LAKE KUTUA YANGA LAWA JEPESI

 

 KLABU ya Horoya leo Julai 18 imetangaza rasmi kusitisha mkataba na mchezaji wao Heritier Makambo.

Kupitia katika ukurasa rasmi wa Horoya ya Guinea wameandika kwamba wanashukuru kwa huduma ya mchezaji huyo ambaye amedumu hapo kwa muda wa misimu miwili.

Nyota huyo aliibuka hapo 2019 akitokea Klabu ya Yanga ambapo alikuwa ni mfungaji namba moja ndani ya Yanga alipotupia mabao 17 na kuwa namba tatu kwa washambuliaji wenye mabao mengi.

Namba moja alikuwa ni Meddie Kagere ambaye alitupia mabao 23 na alisepa na kiatu cha ufungaji bora.

Huenda dili lake la kurudi Yanga likajibu kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi hao ambao wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya pili.

Hivyo kuangwa kwake rasmi na mabosi wake hao kunafanya dili lake kuwa jepesi kuweza kutua Yanga

Post a Comment

0 Comments