Yanga Kupumuzika Wiki Mbili Tu.

 


Uongozi wa klabu ya Yanga unatarajiwa kuwapa mapumziko ya wiki mbili wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi mara baada tu mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Simba mchezo ambao utachezwa July 25 mkoani Kigoma.

Baada ya mapumziko hayowachezaji wote watatakiwa kurudi kambini August 08 kuanza maandalizi (Pre-Season) nchini Morocco ambapo Yanga wamepewa mwaliko na klabu ya Raja Casablanca kwenda kujifunza mambo mbalimbali kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Pia kocha mkuu wa klabu hiyo ameuomba uongozi wa klabu kukamilisha haraka usajili ya wachezaji wapya 8 (4 kimataifa na 4 wa ndani) aliowapendekeza kufikia August 05 ili waende na timu kujiandaa kwa ligi kuu ya Vodacom na Klabu bingwa Afrika kwa msimu wa 2021/22.

Post a Comment

0 Comments