TAARIFA YA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA SHAHADA YA KWANZA KATIKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO PDF.


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na Wadau wote wa Elimu ya juu ndani na nje ya nchi kuwa kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita, Tume imefungua dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza kuanzia leo tarehe 12/7/2021 badala ya tarehe 15/7/2021 iliyokuwa imepangwa awali. Dirisha hili litakuwa wazi hadi tarehe 05/8/2021. 

Tume inawahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU www.tcu.go.tz, tovuti za vyuo vilivyoruhusiwa kudahili wanafunzi wa Shahada za Kwanza, pamoja na taarifa mbalimbali zinazotolewa na TCU kupitia vyombo vya habari.


TAARIFA  YA  KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA SHAHADA YA KWANZA KATIKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO PDF.

Post a Comment

0 Comments