MLINZI wa kulia wa klabu ya Simba, David Kameta ‘Duchu’ huenda akawa sehemu ya kikosi cha klabu ya Mbeya kwanza kitakachoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao kama mchezaji wa mkopo akitokea Simba.
Duchu alisajiliwa na Simba kutokea klabu ya Lipuli mwanzoni mwa msimu huu, lakini amekuwa katika wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza mbele ya beki Mwandamizi, Shomari Kapombe.
Uamuzi huo wa kumtoa kwa mkopo Duchu unatokana na usajili wa mlinzi wa kulia, Israel Patrick Mwenda ambaye taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu.
0 Comments