Aliyoyasema Kocha wa Yanga Kuhusu Usajili Wa Mrithi Wa Metacha

 


KOCHA wa Makipa wa Yanga, raia wa Kenya, Razack Siwa, amefungukia ishu ya kuhitajika kwa mrithi wa Metacha Mnata kwa kusema kuwa, hadi muda huu hajashirikishwa lolote juu ya usajili zaidi yeye ametakiwa kujikita kwenye masuala ya ufundi tu.

Tangu Metacha aliporipotiwa kusimamishwa na klabu hiyo kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, mwezi uliopita, mabosi wa Yanga walikaririwa wakisema wapo kwenye hatua za kutafuta golikipa mpya wa kimataifa.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha wa Makipa wa Yanga, Siwa alisema kuwa, hadi muda huu yeye hana taarifa sahihi juu ya viongozi kusajili kipa mpya, pamoja na kuwepo na hitaji hilo.

“Kusema kweli taarifa za kuongeza kipa mpya nimezisikia tu, ila mimi sijui lolote ni wapi anatoka na atakuja lini, hivyo kazi yangu kwa sasa mimi nimejikita kwenye kufundisha na kama kuna hilo basi tutajua huko mbeleni,” alisema Siwa.

Post a Comment

0 Comments